DUA WAKATI WA KUFUTURU


Inapendeza aliefunga wakati wa kufuturu kuomba dua, kwani wakati wa kufuturu ni wakati ambao dua hazirudishwi hujibiwa, na zinakubaliwa haraka. Hadithi ya Abdallah bin Umar bin Aas R.A.A. kasema, “Kasema Mtume S.A.W., [1] “

إِنَّ لِلصَّائِمِ عِنْدَ فِطْرِهِ لَدَعْوَةً مَا تُرَدُّ.

Maana yake, “Kwa yule aliefunga wakati wa kufuturu dua yake hairudishwi”. Na imethibiti kutoka kwa Mtume S.A.W. kwamba alikuwa akiomba dua wakati wa kufuturu. Hadithi ya Marwan bin Salim kasema, “Kasema Ibn Umar R.A.A., “Mtume S.A.W. wakati wa kufuturu alikuwa akisema,[2]“

ذَهَبَ الظَّمَأُ وَابْتَلَّتِ الْعُرُوقُ وَثَبَتَ الْأَجْرُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ.

Dhahaba dhama`u wabtallatil- uruuqu, wa thabata l`ajru in sha Allah.

Maana yake, “Kiu kimeondoka, na mishipa imerowana, na ujira utapatikana Mungu akipenda.” Pia hadithi nyingine iliyo hadithiwa na Mua`dh bin Zuhrah kasema, “Mtume S.A.W. alikuwa akisema wakati wa kufuturu,[3] “

اللَّهُمَّ لَكَ صُمْتُ وَعَلَى رِزْقِكَ أَفْطَرْتُ.

Allahumma laka sumtu wa ala rizqika aftarutu.

Maana yake, “Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili Yako nimefunga, na kwa riziki Yako nimefuturu.”

Comments

Popular posts from this blog

8 Reasons You Should NEVER Drink Water While Standing