Umuhimu wa kilimo katika Uislam

Wakulima wanakagua shamba lao - Oman

Kasema Allah mtukufu katika kitabu chake.

  وَآيَةٌ لَّهُمُ الْأَرْضُ الْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَاهَا وَأَخْرَجْنَا
مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ 

وَجَعَلْنَا فِيهَا جَنَّاتٍ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ وَفَجَّرْنَا فِيهَا مِنَ الْعُيُونِ
لِيَأْكُلُوا مِن ثَمَرِه وما عَمِلَتْهُ أَيْدِيهِمْ ۖ أَفَلَا يَشْكُرُونَ

Maana yake: 

_na ishara hiyo kwao - ardhi iliyo kufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanazil_

_na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemchem ndani yake_.

_ili wale matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! basi je, hawashukuru?_

Mafunzo yake

Neema nyingi zinatoka ardhini kwa kulima na kuipanda kila aina ya mbengu, hapo Allah sw anatupa habari au anatukumbusha neema ya ardhi tupate kushukuru, kwa kutufanyia mabstani ya kila aina  mizabibu ,mitende, pia chemchem zina chemka kila pande za dunia,ilitupate kula matunda yake alotujaalia Allah sw kwa hio ni juu yetu tulime hii aridhi ili tule kheri zake zisizo hesabika ,akitaka mwanadamu utajiri upo aridhini akitaka umasikini pia upo aridhini atakapoingalia kama tandiko tu bila kuwaza au kuona hekma ya Allah sw,

kasema Mtume s. a.w 

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
 "لو أنكم توكلتم على الله حق توكله لرزقكم كما يرزق الطير تغدو خماصا وتروح بطانا
     " رواه أحمد والترميذي

Maana yake:
kasema mtume wa Allah sw((lau nyinyi _mgelikuwa mwamtegemea Allah ukweli wa kumtengemea au kiukwelikweli basi ange kuruzukuni kama anavyo waruzuku ndege anaamka akiwa njaa hana kitu tumboni mwake (anatoka  hana kitu) na anarudi kwa kiota chake hali yakuwa kashiba))_

Kasema Mtume s a w kwa hadithi nyingine:-

قال رسول اللّٰه صلي اللّٰه عليه وسلّم
من كانت له أرضا فليزرعها فان لم يستطع وعجز عنها فليمنحها اخاه المسلم 

maana yake:'
kasema Mtume wa Allah saw (mwenye kuwa na ardhi basi 
_alime ardhi hio, kama hawezi na akashidwa kufanya hivyo ! basi amsaidie ndugu yake mwislamu alime ardhi hio._

 Faida za kilimo

kupatisha chakula kwa jami. jamii ikijishughulisha na kilimo watapata chakula cha kutosheleza mahitaji yao na wataishi maisha ya raha  na utulivu. 

kutupatia mavazi. kwani mavazi mengi tuvaayo yatokana na kilimo kama vile nguo za pamba. sufi nk

hutuingizia pesa za kigeni. kwasababu wengi wanaojishughulisha na kilimo huuza mazao yao nchi nyingine kama mali ghafi na hapo hupata kuingiza pesa za kigeni. 

.husaidia kuhifadhi uchafuzi wa mazingira.hii ni kwakua mimea ndo chanzo kikuu cha hewa ya oxygen ambayo ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu na wanyama kwani huvuta hewa hii ndo akawa na uhai.

hupendezesha mazingira na maeneo mbali mbali. kwani mwanadamu kwa kiasi kikubwa sana ahitajia kustarehe na kupumbaa kwa miti pale anapoiangalia miti ikiyumba huku na kule

 hupunguza idadi ya wasokua na kazi. kwakua mkulima stadi hawezi kujitosheleza peke yake bali ahitaji usaidizi wakati wa kulima, kubebewa kupelekwa sokoni na kuuza pia, hapo hubidi aajiri wafanyakazi ili atimize malengo yake kwa njia rahisi.

 .husaidia kuboresha masoko kwa bidhaa zingine. kwani mkulima hua ahitajia vifaa ama zana za kumsaidia katika kilimo, kama trekta, jembe,mbolea na kadhalika.

:husaidia kukua na kuongezeka viwanda. tukumbuke viwanda vingi duniani malighafi zake zatokana na kilimo.

husaidia kua na ongezeko la wasomi. kwani jamii ikizingatia kilimo hua ni lazima wapatikane wataalamu wa kilimo.

Hujenga uhusiano mwema na urafiki Kati ya  jamii na jamii nyingine au nchi na nchi nyingine. Mfano nchi zenye utajiri wa mafuta huhitajia wataalamu kwa ajili ya kutoa mafuta mengi na hua ni jambo la dharura zaidi kua na wataalamu walobobea.
Kilimo humtoa binadamu kwenye umasikini na kumwingiza kwenye utajiri kwani matajiri wengi huanzia na mazao.
Kilimo kinatupatia aina mbalimbali za vyakula ambavyo ndo uhai wa binadamu.
Kilimo pia ni miongoni mwa mazoezi kwa wale ambao hajiwezi kutumia nyenzo za kilimo ila ni mikono yao.

MTAARISHAJI
Humoud Al rawahi
             📱+96894646722
  Oman

Comments

Popular posts from this blog

8 Reasons You Should NEVER Drink Water While Standing