SIKU YA ARAFAH

SWAWM YA SIKU YA ARAFAH INAFUTA MADHAMBI YA MIAKA MIWILI Ni fadhila kubwa kwa Waislamu kufutiwa madhambi yao. عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ : ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم Abuu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ( (Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake )) [Muslim] Kufunga Swawm siku ya ‘Arafah ni makhsusi kwa wasiokuweko huko ‘Arafah siku hiyo. Ama mahujaji hawatakiwi kufunga Swawm siku hiyo. SIKU YA KUTAKABALIWA DU’AA Amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ، وخَيْرُ مَا قُلْتُ أنَا وَالنَّبيُّونَ مِنْ قَبْـلِي: لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ،