Maneno ya Wenye hekima


💞 أقْوَال ُ الحُكماَءِ  💞
     📝MANENO YA  📝
     WENYE HEKMA
               💫{{  1004  }}💫
         
           ☆ وَافْعَلُوا خَيْرَاتِ ☆
NA FANYENI YALIYO MEMA✔       
______________🌹▪▪

✍قَالَ أحَدُ مِنَ الحُكمَاءِ
📝Kasema mmoja 
Mwenye HEKMA:'

📘 مَدُحُ النّاسِ لَكَ لَنْ يَدْخٌلَكَ الجَنّةَ

  ✍ Kusifiwa na  Watu kwako haitokuingiza Peponi.(Ukajiona ndio umefuzu)

📕 وَذَمُّ النّاسِ لَكَ لَنْ يُخرِجَكَ مِنَ النار

  ✍ Na kukusema vibaya Watu Haitokutowa wewe  Motoni.(Ukaona ndio umeokoka tena ).

📙 لِذَلكَ لاَ تكُنْ عَبْدًا لِأفوَاهِهِمْ

✍Kwa hivyo usiwe mtumwa kwa kusikiliza Midomo yao tu .(Na huna ulifanyalo na  kutenda yaliyomema )

___________________🎊

     📢☆ ZI NGATIA☆

📝 Matendo Mema yenye Ikhlaas ndio yatakayokukingiza wewe kubaki Peponi Milele.

 Allah anasema:-

( وَمَن يَأْتِهِ مُؤْمِنًا قَدْ عَمِلَ الصَّالِحَاتِ فَأُولَٰئِكَ لَهُمُ الدَّرَجَاتُ الْعُلَىٰ )

طـه (75) Taa-Haa

_Na atakaye mjia naye ni Muumini aliye tenda mema, basi hao ndio wenye vyeo vya juu._

📝 Matendo yako Maovu na Mchafu na ukafa bila toba ndio yatakayokukuingiza wewe udumu milele Motoni.

    Allah anasema:'

( إِنَّهُ مَن يَأْتِ رَبَّهُ مُجْرِمًا فَإِنَّ لَهُ جَهَنَّمَ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ )

طـه (74) Taa-Haa

_Hakika ataye mjia Mola wake Mlezi naye ni mkhalifu, basi kwa yakini, yake huyo ni Jahannamu. Hafi humo wala haishi._

📝Usipendelee kutaka kusifiwa tu bila hata kutenda yaliyo kheri na mema.

   Allah anasema

( لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوا وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا فَلَا تَحْسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٍ مِّنَ الْعَذَابِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ )

آل عمران (188) Aal-Imran

_Usiwadhanie kabisa wale wanao furahia waliyo yafanya, na wakapenda kusifiwa kwa wasiyo yatenda, usiwadhanie kuwa watasalimika na adhabu. Yao wao ni adhabu chungu._

________________☆☆☆

   ✍ MTAARISHAJI 
Humoud Al rawahiy
             📞+96894646722
          Oman   
💫💞💫~~~~~~~~~~

Comments

Popular posts from this blog

Kisomo Cha Quran Tukufu