Posts

Showing posts from September, 2019

Binadamu

MASIKINI MWANAADAMU, KILA SIKU ANAPATWA NA MITIHANI MITATU! Mtihani wa Kwanza; Umri wake unapungua kila siku na wala hajali kwamba siku inapunguza umri wake. Mali yake ikipungua anashughulishwa sana; ambapo mali inarudi; lakini umri haurudi. Mtihani wa Pili. Kila siku anakula riziki ya Allah Taala; kama ni halali, ataulizwa kwa hayo; na kama ni haramu ataadhibiwa kwa hayo; na wala hajali matokeo ya hesabu. Mtihani wa Tatu. Kila siku anaikaribia Akhera kwa kiwango fulani; na anaiacha dunia kwa kiwango fulani; lakini pamoja na hayo; haipi umuhimu Akhera inayo mkaribia kama anavyoipa umuhimu dunia inayo maliza kwake; Na wala hajui mwisho wake ni Pepo au Moto mkali. Kutokana na kughafilika na Tamaa za kidunia na yaliyo kuwemo ... Hali ya kuwa ni mapito mafupi tuu yasio kuwa na faida yoyote huko twendako zaidi ya Amali Njema... Dini ni Nasaha ,,

HII NAYO NI ADABU NJEMA

1. Usimpigie mtu simu kwa zaidi ya mara mbili mfululizo. Ukishaona simu yako haipokel'ewi basi elewa kuna sababu ya msingi acha subiri akupigie pindi atakapoona ulimtafuta. 2. Rejesha pesa ulizokopa bila kusubiri kukumbushwa na aliyekukopesha. Hiyo inaonesha uadilifu wako na tabia yako. Vivyo hivyo rejesha mwamvuri, peni, kitabu au chochote ulichoazima hata kama kidogo usisubiri kukumbushwa. 3. Usiagize chakula cha  gharama kubwa pale unapotolewa out na mtu. Ikiwezekana mwombe akuagizie mwenyewe au shauriana naye chakula gani unaweza kuagiza. 4. Usiulize maswali yenye ukakasi kama "Hee bado hujaolewa/hujaoa tu? Au " he! Hujapata mtoto tu?", "he! Hamjajenga tu? " Mwee bado tu hamjanunua gari?" Kwa kifupi ni kwamba hayakuhusu mhusika akipenda mjadili hilo ataanzisha mwenyewe. 5. Ikitokea unaingia mahali na kuna mtu anakuja nyuma yako ni vizuri ukamshikia mlango bila kujali umri au jinsia yake. Haikugharimu lolote kuonesha unajali. 6. Mkienda mahal