Sala ya Dhuha


Sala ya dhuha ni katika Sala ya Sunna iliyothibiti kutoka kwa Mtume S.A.W.
Kasema Ummu Haani bint Abi Talib,

ﺻَﻠَّﻰ ﺭَﺳُﻮﻝُ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﺻَﻠَّﻰ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻪِ ﻭَﺳَﻠَّﻢَ في بيتى صلاة ﺍﻟﻀُّﺤَﻰ ثماني ركعات ملتحفا في ثوب واحد.

Maana yake,
"Alisali Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W nyumbani kwangu Sala ya dhuha rakaa nane, huku amejifunika nguo moja."

WAKATI WA SALA YA DHUHA NA IDADI YA RAKAA ZAKE.

Wakati wa Sala ya dhuha unaanza baada ya kupanda kwa jua kwa dakika kumi na mbili hivi, na unamalizika kwa kuwepo kwa jua katikati ya mbingu, na kila ikicheleweshwa ni bora zaidi.

Kasema Zaid ibn Arqam,

"Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W alikwenda Quba na akawakuta watu wanasali Sala ya Dhuha akawaambia,

ﺻَﻠَﺎﺓُ ﺍﻟْﺄَﻭَّﺍﺑِﻴﻦَ ﺣِﻴﻦَ ﺗَﺮْﻣَﺾُ ﺍﻟْﻔِﺼَﺎﻝُ.

Maana yake;
"Sala ya wanao rejea kwa Mwenyezi Mungu inasaliwa wakati watoto wa ngamia wanapochomwa na joto jua."

Na sala hii inasaliwa kuanzia rakaa mbili na kuendelea kufuatana na uwezo wa mtu.

Kasema Muadh R.A.A,
"Nikimuuliza Bibi Aisha R.A.A.H,
"Rakaa ngapi alikuwa akisali Mtume S.A.W Sala ya Dhuha? Akasema,

ﺃَﺭْﺑَﻊَ ﺭَﻛَﻌَﺎﺕٍ ﻭَﻳَﺰِﻳﺪُ ﻣَﺎ ﻳَﺸَﺎﺀ.

Maana yake;
"Rakaa nne na anazidisha anavyoweza".

FADHILA ZA SALA YA DHUHA.

Sala ya dhuha ina fadhila sana kama jinsi vile ilivyothibiti kutoka kwa Mtume S.A.W katika hadithi zifuatazo:

Kasema Abu Dhar R.A.A, Kasema Mtume S.A.W

ﻳُﺼْﺒِﺢُ ﻋَﻠَﻰ ﻛُﻞِّ ﺳُﻠَﺎﻣَﻰ
ﻣِﻦْ ﺃَﺣَﺪِﻛُﻢْ ﺻَﺪَﻗَﺔٌ، ﻓَﻜُﻞُّ ﺗَﺴْﺒِﻴﺤَﺔٍ ﺻَﺪَﻗَﺔٌ، ﻭَﻛُﻞُّ ﺗَﺤْﻤِﻴﺪَﺓٍ ﺻَﺪَﻗَﺔٌ، ﻭَﻛُﻞُّ ﺗَﻬْﻠِﻴﻠَﺔٍ ﺻَﺪَﻗَﺔٌ، ﻭَﻛُﻞُّ ﺗَﻜْﺒِﻴﺮَﺓٍ ﺻَﺪَﻗَﺔٌ،
ﻭَﺃَﻣْﺮٌ ﺑِﺎﻟْﻤَﻌْﺮُﻭﻑِ ﺻَﺪَﻗَﺔٌ ، ﻭَﻧَﻬْﻲٌ ﻋَﻦْ ﺍﻟْﻤُﻨْﻜَﺮِ ﺻَﺪَﻗَﺔٌ، ﻭَﻳُﺠْﺰِﺉُ ﻣِﻦْ ﺫَﻟِﻚَ ﺭَﻛْﻌَﺘَﺎﻥِ ﻳَﺮْﻛَﻌُﻬُﻤَﺎ ﻣِﻦْ ﺍﻟﻀُّﺤَﻰ.

Maana yake,
"Inapoingia asubuhi kila kiungo cha mfupa wa kila mmoja wenu kinahitajia kutolewa sadaka, kumsifu Mwenyezi Mungu yaani kusema SUBHANALLAH ni sadaka, na kumshukuru Mwenyezi Mungu yaani kusema ALHAMDULILLAH ni sadaka, na kumpwekesha Mwenyezi Mungu yaani kusema LAA ILAAHA ILLA LLAHU ni sadaka, na kumtukuza Mwenyezi Mungu yaani kusema ALLAHU AKBAR ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka, na yote haya yanatoshelezwa kwa kusali rakaa mbili za DHUHA".

Kasema Abdullah bin Amr bin Al'aas R.A.A.

"Mtume S.A.W alitutuma kwenda vitani na tulipata mateka wengi na kurudi mapema. Watu wakawa wanazungumzia kuhusu ushindi wao wa haraka, na wingi wa mateka waliopata, na kurudi majumbani mwao mapema.

Mtume S.A.W aliposikia akasema,

ﺃَﻟَﺎ ﺃَﺩُﻟُّﻜُﻢْ ﻋَﻠَﻰ ﺃَﻗْﺮَﺏَ ﻣِﻨْﻪُ ﻣَﻐْﺰًﻯ ، ﻭَﺃَﻛْﺜَﺮَ ﻏَﻨِﻴﻤَﺔً ، ﻭَﺃَﻭْﺷَﻚَ
ﺭَﺟْﻌَﺔً ؟ ﻣَﻦْ ﺗَﻮَﺿَّﺄَ ، ﺛُﻢَّ ﻏَﺪَﺍ ﺇِﻟَﻰ ﺍﻟْﻤَﺴْﺠِﺪِ ﻟِﺴُﺒْﺤَﺔِ ﺍﻟﻀُّﺤَﻰ ، ﻓَﻬُﻮَ ﺃَﻗْﺮَﺏُ ﻣَﻐْﺰًﻯ ، ﻭَﺃَﻛْﺜَﺮُ ﻏَﻨِﻴﻤَﺔً ، ﻭَﺃَﻭْﺷَﻚُ
ﺭَﺟْﻌَﺔً.

Maana yake,
"Je nikuelezeni ni kikosi gani kilichofanikiwa haraka zaidi, na kilichopata ngawira nyingi zaidi na kurudi upesi? Ni yule atakaetawadha nyumbani kwake halafu akaenda msikitini kusali Sala ya Al Fajr, kisha akasali sala ya Dhuha, basi hiyo itakuwa vita yenye mafanikio haraka, na yenye ngawira wengi, na kurudi upesi."

Pia Kasema Abu Huraira R.A.A,

ﺃَﻭْﺻَﺎﻧِﻲ ﺧَﻠِﻴﻠِﻲ ، ﺻَﻠَّﻰ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻪِ ، ﺑِﺜَﻼﺙٍ ﻻ ﺃَﺩَﻋُﻬُﻦَّ ﻓِﻲ ﺣَﻀَﺮٍ ﻭَﻻ
ﻓِﻲ ﺳَﻔَﺮٍ  ركعتي الضحى وصومِ ﺛَﻼﺛَﺔِ ﺃَﻳَّﺎﻡٍ ﻣِﻦْ ﻛُﻞِّ ﺷَﻬْﺮٍ ، وأن لا أنام إلا على وتر.

Maana yake;
"Kipenzi changu (Khalil) Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W aliniusia mambo matatu ambayo siyaachi safarini, na wala nikiwa nyumbani:
KUSALI SALA YA DHUHA.
KUFUNGA KILA MWEZI SIKU 3.
NA KWAMBA NISILALE MPAKA NIMESALI SALA YA WITRI.

قُلْ هَٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ.

Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.

Imeandaliwa Na Kufikishwa na:

_Amour Al Habsi._
(+96899420700)
Ukumbi Wa FaidikaNaMawaidha.

_"Jiunge Leo Upate Chakula Cha Roho"_

Comments

Popular posts from this blog

8 Reasons You Should NEVER Drink Water While Standing