Posts

Showing posts from April, 2018

Sala ya Dhuha

Image
Sala ya dhuha ni katika Sala ya Sunna iliyothibiti kutoka kwa Mtume S.A.W. Kasema Ummu Haani bint Abi Talib, ﺻَﻠَّﻰ ﺭَﺳُﻮﻝُ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﺻَﻠَّﻰ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻪِ ﻭَﺳَﻠَّﻢَ في بيتى صلاة ﺍﻟﻀُّﺤَﻰ ثماني ركعات ملتحفا في ثوب واحد. Maana yake, "Alisali Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W nyumbani kwangu Sala ya dhuha rakaa nane, huku amejifunika nguo moja." WAKATI WA SALA YA DHUHA NA IDADI YA RAKAA ZAKE. Wakati wa Sala ya dhuha unaanza baada ya kupanda kwa jua kwa dakika kumi na mbili hivi, na unamalizika kwa kuwepo kwa jua katikati ya mbingu, na kila ikicheleweshwa ni bora zaidi. Kasema Zaid ibn Arqam, "Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W alikwenda Quba na akawakuta watu wanasali Sala ya Dhuha akawaambia, ﺻَﻠَﺎﺓُ ﺍﻟْﺄَﻭَّﺍﺑِﻴﻦَ ﺣِﻴﻦَ ﺗَﺮْﻣَﺾُ ﺍﻟْﻔِﺼَﺎﻝُ. Maana yake; "Sala ya wanao rejea kwa Mwenyezi Mungu inasaliwa wakati watoto wa ngamia wanapochomwa na joto jua." Na sala hii inasaliwa kuanzia rakaa mbili na kuendelea kufuatana na uwezo wa mt