Wanaume na Wanawake wanaojihifadhi Tupu zao


DARSA YA KWANZA

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu): Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aina mbili za watu wa motoni siwaoni; Watu ambao wana fimbo (mijeledi) kama za mkia wa ng'ombe dume ambazo wanawapigia watu, na wanawake ambao wamevaa lakini wako uchi, wanawashawishi wanaume wawatongoze, na wanaelekea kwao (kwa kuwa warahisi). Vichwa vyao kama nundu za ngamia zinazoyumba. Hawataingia Peponi wala hawatasikia harufu yake ingawa harufu yake inaweza kunuswa kutoka masafa kadhaa na kadhaa)) [Muslim]  

Hadiyth hiyo ya Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inatudhihirikia uhakika wake kwani tunawaona dada zetu wengi wakidhani kuwa wamevaa mavazi ya hijaab na hali hawakutimiza hijab ya sheria inavyopasa. Utamuona mwanamke amejifunika kichwa tu lakini mwili wake wote haukusitirika kutokana na mavazi aliyovaa. Hivyo hudhani kuwa hijaab hasa ina maana ya kujifunika nywele pekee.

Basi hebu tutaje hapa hijaab ya Kiislamu inayotakikana kisheria:

1.  Nguo iwe ndefu ya kukufunika mwili mzima mpaka miguu, na kama ni fupi kidogo basi uvae soksi. Ukivaa nguo ambayo itaonyesha sehemu yoyote ya mwili isipokuwa uso na viganja, basi utakuwa hukuvaa hijaab sawa sawa

2.    Nguo hiyo iwe pana na sio yenye kuonyesha umbo lako, yaani isiwe yenye kukubana popote mwilini khaswa kuanzia kifuani hadi magotini.

3.    Nguo iwe nzito na si nyepesi yenye kuonyesha mwili wako, yaani kitambaa cha nguo kisiwe chepesi.

4.    Kutokuvaa nguo zinazofanana na nguo za kiume.

5.    Kutokuvaa nguo zenye urembo sana za kuvutia  

6.    Kutotia manukato.

Dada zetu wa Kiislamu watakapotimiza haya watakuwa wamekamilisha hijaab zao na watakuwa katika stara pamoja na kusitiri jamii na ndipo watakapokuwa wamejitahidi kujihifadhi waweze kuingia katika sifa hiyo ya kuhifadhi tupu zao Insha Allah.```

Itaendelea In shaaa ALLAH

*☎+97433799776*

NDOA KATIKA UISLAM
📗〽〽〽〽〽〽〽〽〽📗

Comments

Popular posts from this blog

8 Reasons You Should NEVER Drink Water While Standing