Faida za sadaka

Laiti mtoa sadaka angejua kwa yakini kwamba sadaka yake inapitia kwenye (mkono) wa Mwenyezi Mungu kabla ya kuingia mkononi mwa masikini, ingekuwa ladha ya mtoaji.. ni kubwa kuliko ladha ya mpokeaji..
  -ibn alqayyim

Je unajua faida ya kutoa sadaka?
Sikilizeni enyi watoa sadaka, nyinyi na ambao wanasaidia kufikisha sadaka..

1- Sadaka ni mlango miongoni mwa milango ya pepo

2-Sadaka ni bora ya matendo mema, na sadaka bora ni kulisha chakula

3- Sadaka inamfunika kivuli mtoaji na inamuondosha kwenye moto

4-Sadaka inazima ghadhabu za Mola na joto la kaburi

5- Sadaka ni jambo bora la kumzawadia maiti na inamfaa zaidi, na Mola anaitunza

6-Sadaka ni usafisho, na utakaso wa nafsi na huongeza mema

7- Sadaka ni sababu ya furaha kwa mtoa, na ni sababu ya kung'ara uso wake siku ya kiama

8- Sadaka inaleta amani kutokana na hofu siku ya fazaa kubwa, na humfanya mtoa sadaka asipatwe na huzuni

9- Sadaka ni sababu ya kughufiriwa dhambi na kusamehewa makosa

10- Sadaka ni miongoni mwa bishara za mwisho mwema na sababu ya dua ya Malaika

11- Mtoa sadaka ni mbora wa watu, na sadaka thawabu zake ni kwa kila aliyeshiriki

12- Mwenye kutoa sadaka ameahidiwa kheri nyingi na ujira mkubwa

13- Kutoa ni miongoni mwa sifa za wacha Mungu, na sadaka ni sababu ya mapenzi ya waja wa Mola kwa mtoa sadaka

14- Sadaka ni ishara miongoni mwa ishara za ukarimu na alama miongoni mwa alama za ukarimu na wema

15- Sadaka ni sababu ya kukubaliwa dua na kuondoshewa matatizo

16- Sadaka inaondoa balaa na inaziba milango sabini ya mabaya ya dunia

17- Sadaka inazidisha umri na mali, na ni sababu ya riziki na nusra

18- Sadaka ni ponya, dawa, na shifaa

19- Sadaka inazuia moto, gharika, wizi, na inazuia kifo kibaya

20- Sadaka ujira wake ni ule ule  japo ukitoa kwa wanyama au ndege..

Na sadaka bora ni ile unayoifanya sasa.. ni kueneza maneno haya kwa nia ya sadaka kwani kila anayetekeleza maneno haya na akawafundisha wanaokuja, basi ujira wake uko kwa Mola wake kwa idhini yake

Comments

Popular posts from this blog

8 Reasons You Should NEVER Drink Water While Standing