Dunia
﴿ ﺑِﺴْﻢِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤﻦِ ﺍﻟﺮَّﺣِﻴﻢِ ﴾
💎Maneno ya Dhahabu💎
(23)
🌍 WAKISHINDANA KWA DUNIA, SHINDANA NAO KWA AKHERA
🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹
إذا رأيت الناس يتنافسون في الدنيا فنافسهم في الآخرة
_Ukiwaona watu wanashindana kwa kuitafuta dunia, Basi washinde kwa kuitafuta na kuikimbilia akhera._
Allah ﷻ anasema:
{وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۖ وَلَلدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ}
```Na maisha ya dunia si chochte ila ni mchezo na pumbao tu. Na hakika nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wanao mcha Mungu. Basi, je, hamtii akilini?```
🌎DUNIA NI MAPITO TU:
فإنما تذهب دنياهم وتبقى الآخرة.
```Kwa hakika na bila shaka wala si vinginevyo, dunia yao itaondoka na akhera itabakia daima```
Allah ﷻ anasema:
{وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ}
```Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.```
(Al aalaa 17)
■ FANYA WINGI WA KUKUMBUKA MAUTI
ما ألزم عبد قلبه ذكر الموت إلا صغرت الدنيا عليه.
_Hawi mja mwenye kuulazimisha moyo wake kukikumbuka kifo, ila kwake dunia itakua ni kitu kidogo sana tena kisicho na thaman kabisa._
⛔ OLE WAO WATAKAO ATHIRIKA NA DUNIA
{فَأَمَّا مَنْ طَغَىٰ}
```Basi ama yule aliye zidi ujeuri,```
{وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا}
```Na akakhiari maisha ya dunia```,
_{فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَىٰ}_
```Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!```
(Annaziat 37 - 39)
➖➖➖➖➖➖➖➖
CHAGUO NI LAKO SASA
Mrisho Maulid Othman
📱+255655559911
Ukumbi Wa Faidika Na Mawaidha.
الدعوة إسلامية
Jezaka'Allahu kheiry ��
ReplyDelete