Mwaka mpya, nguvu mpya


Mambo ambayo Tunatakiwa Kujiepusha Nayo katika maisha yaliyobakia;
1-Kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama kufanya uchawi, kuwaendea waganga, watabiri, kutufu makaburini, na mengineyo ya shirki
2-Kuzini
3-Kulewa
4-Kuiba na kumdhulumu mtu haki yake
5-Kugombana, kutukanana, kuvunjiana heshima, kudharauliana n.k.
Kusengenya (Ghiybah).
Tv-Kusema uongo, na kila aina ya uovu mwengine.
Mambo ambayo Tunatakiwa Kuzidisha Kutenda;
1- Swalaah na Swalaah za Sunna.
2-Kufunga Swawm Jumatatu na Alkhamiys, Masiku meupe (Ayyaamul-biydhw) (tarehe 13, 14 na 15) na Swawm ya Nabiy   Daawuwd (kufunga kila baada ya siku moja).
3-Kutafuta ‘ilmu ya Dini kwa kusoma na kusikiliza mawaidha.
4-Kuomba maghfirah na kutubia (tawbah).
5-Kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa wingi kwa tasbiyh (Subhaana Allaah), tahmiyd (AlhamduliLLaah) tahliyl (laa ilaaha illa Allaah takbiyr (Allaahu Akbar).
6-kusoma Qur-aan, kumshukuru na kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
7-Kuunga undugu, kwa kuwasiliana na ndugu, jamaa na kila anayemuhusu mtu kwa damu.
8'Kuwafanyia ihsaan wazazi wawili.
9-Kuwafanyia ihsaan majirani, marafiki na Waislamu kwa ujumla.
10-Kutoa Swadaqah.
11-Kulisha maskini.
12-Kusuluhisha waliokhasimikiana.
13-Kuamrishana mema na kukatazana maovu.
Amali njema yoyote ile usiache kuitekeleza ee ndugu Muislamu hata   iwe   ndogo vipi kwa sababu hujui* *‘amali ipi itakayokupatia radhi za Allaah (‘Azza wa Jalla)ikawa sababu ya kuingia kwako Jannah. Kumbuka Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Imepokelewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Usidharau kufanya jambo jema lolote lile hata ikiwa kukutana na nduguyo kwa uso wa bashasha))
[Muslim]
(Mwaka mpya nguvu mpya).
Imani haizeeki.
fikishwa yaliyofikishwa.
Mkono kwa Mkono Hadi Peponi.
Sheikh Rashid Anaomba tubadilike.

Comments

Popular posts from this blog

8 Reasons You Should NEVER Drink Water While Standing