Go Back   Sekenke Forums. > Ukumbi wa Sekenke > Mapishi

Reply
 
Thread Tools Search this Thread Display Modes
Old 05-01-2008, 09:26 AM   #1
alrashdy@68
Senior Expert Member
 
alrashdy@68's Avatar
 
Join Date: Aug 2007
Location: Oman
Posts: 176
Default JINSI YA KUPIKA PIZZA YA KUKU.


WIKI iliyopita katika safu yetu ya mapishi tulielezea jinsi ya kupika choroko, watu wengi walituma maoni yao akiwamo mmoja wa wasomaji wetu ambaye alipenda tumwlekeze jinsi ya kupika pizza.

Pizza nia aina ya kitafunwa kinachotumiwa na watu tofauti na zipo aina mbalimbali ya pizza kulingana na matakwa ya mlaji.

Kuna pizza ya mboga mboga, ya nyama ya kuku na ng’ombe, zote hizi huliwa kulingana na matakwa ya mlaji.

Katika safu yetu leo tutawaletea jinsi ya kupika pizza ya nyama ya kuku.

Mahitaji
Unga wa ngano kilo 1
Chumvi gramu 0.003
Sukari gramu 0.003
Hamira gramu 0.0125
Maji lita moja
Mafuta ya kula
Nyama ya kuku steki ambayo imesagwa
Tomato sauce
Kitunguu maji
Pilipili hoho
Jibini aina ya mozarella
Bakuli kubwa
Jiko (oven)
Kibao cha chapati

Jinsi ya kupika

Chukua unga na weka katika bakuli na changanya na hamira, chumvi, na sukari, kanda unga kama unavyokanda unga wa chapati au maandazi.

Ukimaliza kufanya hivyo weka maji na kisha endelea kukanda unga huo ili uchanganyike vizuri, changanya unga huo kwa muda wa dakika mbili ili uchanganyike na kulainika vizuri.

Ukimaliza kufanya hivyo, weka mafuta katika mchanganyiko wa unga na kisha endelea kukanda kwa muda wa dakika mbili tena na baada ya hapo kata unga huo katika madonge kama jinsi unavyofanya wakati wa kupika chapati.

Ukimaliza kufanya hivyo, sukuma madonge hayo ili yawe katika mfumo wa chapatti na ukimaliza kufanya hivyo chukua uma na toboa chapati hiyo ili kuweka matundu ambayo yatafanya viungo kuingia katika pizza hiyo. Matundu hayo yasitokee upande wa pili.

Hiyo ni hatua ya awali kabisa katika upikaji wa pizza. Tutaendelea sehemu ya pili wiki ijayo.


Last edited by Mahmoud; 05-22-2008 at 11:13 PM.
alrashdy@68 is offline   Reply With Quote
Old 05-01-2008, 09:31 AM   #2
manga
professional
 
manga's Avatar
 
Join Date: Apr 2007
Posts: 413
Default

Asante Ndugu alrashdy@68...
manga is offline   Reply With Quote
Old 05-05-2008, 06:32 PM   #3
alzahraa
Super Moderator
 
alzahraa's Avatar
 
Join Date: Jul 2007
Location: United Arab Emirates
Posts: 438
Default

shukran Alrashdy............Allah akujaze kheiri daima Inshaallah............
__________________
Allah atupe kinga kwa kila hatari.........Baraka kwa kila jambo..............Jibu kwa kila maombi.............Tabasam kwa kila chozi........Atujalie imani na subra katika maisha yetu......Aaaminn................................. ..............

alzahraa is offline   Reply With Quote
Old 04-14-2009, 08:23 PM   #4
Mahmoud
Administrator
 
Mahmoud's Avatar
 
Join Date: Dec 2006
Location: Oman
Posts: 2,010
Default

Shukran Wa baarakallahu fiik na salaam nyingi kutoka kwangu
__________________Mahmoud is offline   Reply With Quote
Reply

Thread Tools Search this Thread
Search this Thread:

Advanced Search
Display Modes

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off

Forum Jump

Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
kuku ummzakaria Uliza tafsiri za ndoto kwa Sheikh Rashid. 1 07-13-2011 06:05 PM
Biriani La Kuku. ahmed Mapishi 3 04-22-2009 08:40 PM
How to Cook Pizza on a Gas BBQ Mahmoud Mapishi 1 03-11-2009 12:58 AM
Microwave Oven with a Pizza Drawer Underneath Mahmoud Hoja mchanganyiko. 1 02-21-2009 02:20 AM
Pilau Ya Kuku Mordiy Mapishi 2 02-02-2009 01:59 PM


All times are GMT +4. The time now is 09:24 AM.

Powered by vBulletin® Version 3.8.3
Copyright ©2000 - 2016, Jelsoft Enterprises Ltd. Mahmoud Al-Asmi