Go Back   Sekenke Forums. > Ukumbi wa Sekenke > Afya na tiba

Reply
 
Thread Tools Search this Thread Display Modes
Old 10-18-2011, 06:30 AM   #1
mzizimkavu2009
Senior Expert Member
 
Join Date: Dec 2009
Posts: 123
Thumbs up Maradhi yanayomsibu binaadamu na tiba yake

Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuhu

MARADHI YANAYOMSIBU BINAADAMU NA TIBA YAKE

A. MATATIZO YA MZIO (ALLERGY). MATATIZO mengi kuhusu maradhi katika mfumo wa kupumua hutokana na hisia kali sana dhidi ya baadhi ya vitu.Vitu hivi baadae humsababishia madhara maarufu kwa jina la Allergy. Mfano wa vitu

hivi ni: pamoja na baadhi ya vyakula; Kufisidika au kuharibika kwa maji (water pollution); Kufisidika au kuchafuka kwa hewa, kwa mfano vumbi (air

pollution); Mabadiliko ya hali ya anga au hewa na mabadiliko ya hali ya misimu; Kemikali, gesi, harufu mbaya au uvundo, moshi; Dawa za kumeza. Mafuta mazuri, hata harufu ya vipodozi au manukato; Na baadhi ya vitu vingine, ambavyo mtu havipendi na pengine humdhuru. Vumbi yaweza kusababisha mtu kupiga chafya,

baridi au moshi vinaweza kumfanya mtu kukohoa, kula baadhi ya vitu vinaweza kumfanya mtu kupata maradhi ya ngozi, kunusa au kupata harufu ya baadhi ya mafuta mazuri yanaweza kumfanya mtu aumwe na kichwa n.k. Hali zote hizi ni mifano ya mzio. Tiba kubwa ya mzio ni kuepukana na yale yote yanayosababisha mzio.

B. PUMU (ASTHMA): Haya ni maradhi ambayo husibu mapafu na kumsababisha mgonjwa apate shida ya kupumua. SABABU: Yawezekana kusababishwa na vumbi, aina ya unga au vumbi litokanalo na maua, baadhi ya vyakula, mabadiliko ya hali ya hewa, wanyama kama paka na mbwa, aina ya bacteria, kuvuta sigara, pumu ya kurithi. n.k. DALILI: (3) Mgonjwa hupata shida ya kupumua ndani

hewa safi ya oksijeni na kupumua nje hewa chafu ya kabondayoksaidi. (4) Wakati mwingine utamsikia mgonjwa akipumua anatoa sauti isiyokua ya kawaida (wheezing sound) hii ni kwa sababu ya wingi wa makohozi (mafua) yaliyosongamana ndani ya mapafu na kuzuia nafasi ya hewa. Mgonjwa hupata shida anapokua ndani ya chumba ambacho ndani yake hakuna hewa ya kutosha kwa sababu ya udogo au upungufu wa madirisha. Mgonjwa hupata nafuu baada ya kutoa na kutema makohozi na kukaa sehemu yenye hewa safi.


(5) Kukohoa au kikohozi cha muda mrefu. TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua bakuli yenye maji ya moto kisha udondoshee ndani yake matone kadhaa ya mafuta ya habatsoda. Kaa juu ya kiti halafu ujifunike shuka na usogeze bakuli lenye maji ya moto na

habat soda ili upate mvuke wake. Tiba hii inaitwa Aromatherapy. Baada ya kufanya hivyo jipake mafuta ya habat soda mgongoni na kifuani halafu unywe mafuta ya habat soda matone matatu. Tumia kanuni hii kutwa mara mbili asubuhi na jioni kwa muda wa wiki mbili. Kanuni ya pili: Chukua asali nusu lita, juisi ya kitunguu saumu mili lita 200, unga wa habat soda vijiko vinne vikubwa, unga wa tangawizi vijiko viwili vikubwa, unga wa mdalasini kijiko kimoja kikubwa. Vyote changanya pamoja. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara tatu.

C. MAFUA (FLU NA COMMON COLD). HAYA ni maradhi maarufu, ambayo huambukiza kwa urahisi kutoka kwa mgonjwa hadi kwa mtu mwingine. TIBA: Chukua asali robo lita, unga wa tangawizi vijiko viwili vikubwa, unga wa mdalasini kijiko kimoja

kikubwa na unga wa habasoda vijiko viwili vikubwa. Changanya zote pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara tatu.

D. MATATIZO YA MASIKIO: Bila shaka viungo au mishipa ya masikio, pua na koo yameungana na yana uhusiano wa karibu. Kwa hivyo kiungo kimoja kikiathirika yawezekana viungo vingine kuathirika, ikiwa vishambulizi vya bacteria vitasambaa hadi sehemu nyingine. Sikio ni kiungo maalum katika viungo vya hisia ambayo kazi yake ni kusikia.
mzizimkavu2009 is offline   Reply With Quote
Old 10-18-2011, 06:31 AM   #2
mzizimkavu2009
Senior Expert Member
 
Join Date: Dec 2009
Posts: 123
Default

MAUMIVU YA MASIKIO NA SABABU ZAKE: Maumivu yoyote ya meno, ufizi na koo yanaweza kusababisha maumivu ya sikio kwa sababu ya mahusiano ya karibu. Pia kukohoa sana kwa muda mrefu kunaweza kusababisha maumivu ya masikio. Sikio linaweza kuuma ikiwa mara kwa mara utaweza kutia vijiti sikioni kwa ajili ya kusafisha.

Wakati mwingine sikio linaweza kushambuliwa na bacteria na kusababisha maumivu.
KUTOKWA NA USAHA SIKIONI: Ikiwa utaweka kitu kama ujiti wa kiberiti au mfano wake sikioni, unaweza kusababisha jeraha kwenye sikio na damu kuanza kutoka. Baadae usaha unaweza kutungwa sehemu ya jeraha na kutoka kidogokidogo. Lakini pia mashambulizi ya bacteria sikioni yanaweza kusababisha kutokwa na usaha.

TIBA ZA MAUMIVU YA MASIKIO NA KUTOKWA NA USAHA: Kanuni ya kwanza: Chukua maji masafi ujazo wa kijiko kimoja cha chai halafu uchukue chumvi kidogo kiasi cha vidole viwili uchanganye ndani ya maji hayo kisha hayo maji uchanganye na asali kijiko kimoja kidogo cha chai. Weka tone moja ya dawa hii ndani ya sikio

lenye kuuma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu. Kanuni ya pili: Dondoshea tone moja ya mafuta ya kitunguu saumu ndani ya sikio ambalo linauma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu.. Kanuni ya tatu: Chukua mafuta ya habat soda na ufanye kama kanuni ya pili. Kanuni ya nne: Ikiwa maradhi ya sikio ni kwa ajili ya bacteria, kunywa antibayotiki asilia kama vile juisi ya Aloe vera, kitunguu saumu, n.k. E.


MATATIZO YA MACHO: KONJACTIVA (CONJUCTIVITS): Ni maradhi ya macho sehemu ya utando au ute sehemu ya conjuctiva, ambayo inaunganisha sehemu ya ndani ya jicho na kope. SABABU:


Yanaweza kusababishwa na vumbi, moshi, upepo ulio na ubaridi, kuweza kutumia macho kwa muda mrefu kutizama kwa mfano kusoma, kukaa katika mwanga mkali wa jua, upepo wenye ukavu na ujoto wenye hali ya umoto, mvuke, gesi, moto, kemikali, n.k. DALILI: Kujikuna, kuvimba

macho, macho kuwa mekundu, macho kutoa maji au machozi, kuhisi kuna mchanga ndani ya macho, kuogopa mwanga mkali, n.k. TIBA: Weka macho yawe safi na uyakoshe kwa maji ya baridi. Epusha macho kutokana na joto, baridi, moshi, vumbi, macho yasitumie nguvu sana kama vile kusoma sana. Tumia dawa za kulainisha choo ikiwa hupati choo vizuri kwa sababu pia huchangia katika maumivu ya kichwa na macho.

F. MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION): Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa. Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo. SABABU ZA MARADHI HUSIKA: (1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B. (2) Maradhi ndani ya utumbo mpana. (3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano. (4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga. (5) Kutokunywa maji ya kutosha. (6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi. (7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo. TIBA: Kanuni ya kwanza:

Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.

Kanuni ya pili: Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asalirobo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.

Kanuni ya tatu: Asali robo lita, na Unga wa Arki susi vijiko vinne vikubwa. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara mbili. Kanuni ya nne: Kunywa kwa wingi maji ya kunywa ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga.


Kanuni ya tano: Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini. H.

MARADHI YA KUHARISHA:MARADHI ya kuharisha ni maradhi ambayo mgonjwa hupata haja kubwa mara kwa mara na haja kubwa huwa laini na wakati mwingine huambatana na gesi au maumivu. SABABU ZAKE: (1) Kula chakula kichafu. (2) Kula chakula kilichoingia viini vya maradhi.

TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua kijiko kimoja cha Maua ya babu naji (chamomile) ukoroge ndani ya kikombe cha chai na maji ya moto. Yakishapoa unywe bila ya kuongeza sukari.Fanya hivyo kutwa mara tatu. Ndani ya babunaji mna virutubisho vyenye uwezo wa kusitisha kuharisha.

Kanuni ya pili: Chukua anisuni (aniseed) kijiko kimoja kidogo uweke ndani ya kikombe kimoja cha chai cha maji ya moto yaliyochemka kisha ukoroge. Wacha dawa ikae ndani ya maji dakika tano kisha uchuje halafu uongeze asali kijiko kimoja. unywa kikombe kimoja kutwa mara mbili. Zaidi ya hayo, tukuweke wazi tu kuwa, dawa hii pia huvipa nguvu jamii ya viungo vya kulia chakula.

Kanuni ya tatu: Chukua majani ya nanaa (Mint)na utayarishe dawa kama mfano wa hapo juu kuhusu anisuni.

Kanuni ya nne: Chukua zaatar na uandae dawa kama mfano wa hapo juu kuhusu majani ya nanaa na anisuni


Kanuni ya tano: Changanya kijiko kimoja cha mafuta ya habat soda ndani ya glasi moja ya maziwa ya mtindi unywe glasi moja kutwa mara mbili.

Maradhi ya KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA: Hali ya kujisikia kuwa unataka kutapika lakini hutapiki inaitwa kichefuchefu (Nausea). Hali hii ni kawaida sana hasa wakati unaposafiri kwa chombo kama meli au ndege, hali ya ujauzito,kupata harufu mbaya, kuona au kuhisi kinyaa baada ya kuona kitu au chakula Fulani kibaya chenye ladha na harufu mbaya, wengine hupata kichefuchefu akimuona mtu mwengine akitapika. Hali ya kichefuchefu humsababishia mtu kuweza kutapika wakati mwingine.

TIBA: Chukua kijiko kimoja kidogo cha unga wa pilipili manga ukoroge ndani ya glasi moja ya maji halafu ukamulie ndani yake ndimu nusu. Kunywa glasi moja kutwa mara tatu.
mzizimkavu2009 is offline   Reply With Quote
Old 10-18-2011, 06:31 AM   #3
mzizimkavu2009
Senior Expert Member
 
Join Date: Dec 2009
Posts: 123
Thumbs up

GESI TUMBONI (COLIC): Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo.

TIBA: Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.


Kutibu Maradhi ya BAWASIRI (MGORO): Haya ni maradhi ambayo humsibu mgonjwa sehemu ya haja kubwa ambayo humsababisha kupata maumivu. DALILI ZAKE: (1) Kupata choo kigumu. (2) Kutokwa damu sehemu ya haja kubwa baada ya kujisaidia. (3) Muwasho au maumivu na joto kali sehemu ya bawasiri. (4) Kupata maumivu wakati unapokaa. (5) Vidonda au kutokwa nje na kijinyama sehemu ya kutokea haja kubwa. (6) Upungufu wa nguvu za kiume.

TIBA: Jambo la kwanza kabla ya tiba mgonjwa aweze kutibiwa maradhi ya kutopata choo vizuri ikiwa anayo kwa sababu huzidisha maradhi haya. Pia epuka kula Nyama hasa ya ngombe, Pilipili na vitu vikali. Halkadhalika usinywe maziwa kwa wingi.

Kanuni ya kwanza: Kunywa juisi ya tikiti maji asubuhi kabla ya chakula na usiku kabla ya kulala.Dawa hii hutibu na kuondoa maumivu ya bawasiri.
Kanuni ya pili: Chukua asali nusu lita , unga wa kamun aswad vijiko vitatu vikubwa,unga wa Habat soda vijiko vitatu vikubwa na unga wa kamun abyadh vijiko viwili vikubwa. Vitu vyote hivi vichanganye pamoja kwa kuvikoroga kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vikubwa vya mchanganyiko huu kisha ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa uchuje halafu unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Ikiwa ni bawasiri ya kutoka nje au yenye vidonda, paka mafuta ya nyonyo au mafuta ya lozi. L.

Maradhi ya VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS): Haya ni maradhi ambayo hufanya vidonda upande wa ndani ya ukuta wa tumbo. Kuna Duodenal ulcer na Gastric ulcer.

DALILI: (1) Kupata maumivu makali chini ya kifua kwa
upande wa ndani. (2) Kuchoka bila sababu. (3) Kuumwa kwa mgongo au kiuno. (4) Kupungua kwa nguvu za kiume. (5) Kuwa na kichefuchefu baadhi ya wakati. (6) Kuwa na kiungulia . (7) Tumbo kujaa gesi. (8) Tumbo kuwaka moto. (9) Kukosa choo na wakati mwingine kupata choo kigumu kama cha mbuzi. (10) Kukosa hamu ya kula. (11) Kutapika damu au wakati mwingine kutapika nyongo. (12) Maumivu makali baada ya kula vitu vikali au chakula cha moto.

TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua asali robo lita uchanganye na unga wa arki susi vijiko vinne vikubwa kisha ukoroge kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vikubwa vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara tatu.

Kanuni ya pili: Chukua viazi vya mviringo (vya chipsi) kama vitatu halafu uvikoshe na kuvimenya. Baada ya kuvimenya upate juisi yake kwa kuvisaga kwenye blenda. Kunywa vijiko vitatu vikubwa vya chakula kutwa mara mbili. Kanuni ya tatu: Chukua lozi gramu 30 halafu usage iwe unga. Changanya lozi hii yote ndani ya kikombe kidogo cha maziwa ya moto kisha uongeze asali vijiko viwili vikubwa. Kunywa kikombe kimoja robo saa kabla ya kula chakula cha asubuhi. Fanya hivyo kwa muda wa mwezi na utapata shifaa.

MATATIZO YA HEDHI: Matatizo ya Hedhi

Matatizo ya Hedhi yanawagusa moja kwa moja wanawake, tena yako katika aina na namna tofauti; hata hivyo nayo yana tiba yake inayolingana na aina ya tatizo husika.

TIBA YA HEDHI ILIYOFUNGA (AMENERRHOEA): Kanuni ya kwanza: Tafuna ufuta kiasi cha kijiko kimoja kila siku mara tatu. Fanya hivyo hadi upate hedhi. Ni bora zaidi kula ufuta kabla ya zile siku ambazo hedhi hutoka na uendelee wakati inapotoka hedhi. Dawa hii ni hatari kwa mwanamke mja mzito, hivyo atahadhari nayo,na tangu hapoyeye haimuhusu. Kanuni ya pili: Chukua Harmal gramu 50, uchemshe ndani ya

maji lita moja. Ikishapoa uichuje. Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara mbili kwa muda wa siku tatu.

TIBA YA HEDHI ISIYOTOKA VIZURI: Chukua Jirjir (rocket) kijiko kimoja ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa uchuje.Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara tatu.
TIBA YA HEDHI INAYOTOKA KWA WINGI ZAIDI YA ADA: Kanuni ya kwanza: Chukua kijiko kimoja cha maua ya Babunaji (Chamomile) ukoroge ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto. Yakishapoa, unywe kikombe kimoja kutwa mara tatu kabla ya kula.

Kanuni ya pili: Chukua zaatar kijiko kimoja kikubwa cha chakula ukoroge ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto. Kunywa kikombe cha chai kutwa mara tatu.

TIBA YA MAUMIVU YA HEDHI YANAYOTOKA KIDOGOKIDOGO (DYSMENORRHOEA): Kanuni ya kwanza: Chukua nanaa na utayarishe mfano wa chai Kunywa kikombe kimoja cha chai kutwa mara tatu

Kanuni ya pili: Chukua mvuje wa kidonge (kidonge kimoja ) na unga wa pilipili manga gramu 50. Weka dawa hizi mbili ndani ya glasi moja ya maji kisha uifunike na uiache ilowane. Bila ya kuchuja kunywa kijiko kimoja kikubwa kutwa mara moja .Rudia tena kunywa siku ya pili ikiwa hujapata mabadiliko.Dawa hii huzibua hedhi iliyoganda au kufunga.

TIBA YA HEDHI INAYOCHELEWA KUTOKA KWA SIKU ZAKE AU KUTOKA KABLA YA SIKU ZAKE KUFIKA: Hapa maana yake ni kuwa baina ya hedhi mbili huenda yakakaribiana sana au kuachana sana kinyume na ada. Yaani siku za tarehe zake haziendi sawa Chukua bakdonise (parsley) gramu 50 kisha uweke ndani ya maji lita moja, ichemshe kwa muda wa dakika tano na ikishapoa uchuje. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili.

MATATIZO YA MKOJO: UCHAFU kutoka mwilini hutolewa nje ya mwili kwa mfumo wa mkojo, kinyesi, jasho kupitia kwenye ngozi. Ikiwa kutatokea kizuizi chochote cha kuzuia uchafu kutoka mwilini sumu ya uchafu huu baadae huchanganyikana na damu na kusababisha maradhi mbalimbali.Figo ni kiungo ambacho hutoa sumu mwilini kupitia njia ya mkojo. VIJIWE VYA KIBOFU CHA MKOJO (DYSURIA): Maradhi haya hutokea kwa kupatikana vijiwe kwenye kibofu cha mkojo. Vijiwe hivi huzuia mkojo kutoka vizuri na kufa yatoke matone matone.


SABABU: (1) Kula nafaka mbichi kwa mfano: mchele, mahindi, njugu karanga, n.k. (2) Vyakula vilivyoisha muda wake wa matumizi au vyakula vyenye viwango vya chini ambavyo havistahiki kuliwa na binadamu. (3) Vyakula vigumu ambavyo tumbo haliwezi kusaga vizuri na hata likisaga, litasaga kwa mashaka kwa mfano chakula ambacho hakijaiva vizuri au nyama ngumu. (4) Kutotafuna chakula vizuri kwa sababu ndani ya tumbo hamna meno, kwa hivyo utalipa tumbo kazi ya ziada.

TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua mbegu za matango vijiko vitano vikubwa na mbegu za tikiti maji vijiko vitano vikubwa uchemshe kwenye maji robo lita. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili.

Kanuni ya pili: Chukua nusu kijiko cha chai cha unga wa sufa , unga wa sukari mawe na unga wa shubiri sokotori(dukani). Vyote vichanganye pamoja. Bugia kijiko kimoja kidogo halafu unywe maji glasi moja asubuhi kabla ya chakula na usiku kabla ya kulala.


MKOJO AMBAO HAUTOKI AU HUTOKA MATONE: Kanuni ya kwanza: Chukua kikombe kimoja cha uji wa ngano uchanganye na kijiko kimoja kidogo cha unga wa uwatu na kijiko kimoja kikubwa cha samli safi ya ngombe. Koroga kwa kijiko. Kunywa kikombe kimoja kutwa mara mbili. Dawa hii hutibu mkojo ambao hautoki au hutoka matone madogo.

MARADHI YA KUTOKWA KWA MKOJO KWA WINGI BILA YA KHIARI (POLYURIA): Haya ni maradhi ya kutokwa na mkojo bila ya khiari . Kabla mkojo haujakusanyika vizuri kwenye kibofu cha mkojo na mgonjwa kujiandaa kwenda

chooni, hutokwa na mkojo hata kabla ya kufika chooni. SABABU: (1) Kulegea kwa kibofu cha mkojo. (2) Maradhi ya kisukari. (3) Kuwa na minyoo tumboni. (4 Kutumia madawa ambayo huchochea kutokwa kwa mkojo. (5) Kuwa katika mazingira au hali ya hewa ya baridi. (6) Kunywa kwa wingi vinywaji, pombe,n.k.

TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua kijiko kimoja kidogo cha chai cha unga wa harmal, vijiko viwili vikubwa vya unga wa tangawizi,kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na vijiko viwili vikubwa vya unga wa pilipili manga. Vichanganye vyote pamoja. Changanya kijiko kimoja cha chai ndani ya kikombe cha maji ya moto ukoroge na yakishapoa unywe kikombe kimoja
mzizimkavu2009 is offline   Reply With Quote
Old 10-18-2011, 06:32 AM   #4
mzizimkavu2009
Senior Expert Member
 
Join Date: Dec 2009
Posts: 123
Thumbs up

KUTOKWA KWA MKOJO KWA WINGI BILA YA KHIARI (POLYURIA): dawa yake hiyo kutwa mara mbili asubuhi kabla ya chakula. Kanuni ya pili: Pika majani ya matango kisha unywe robo kikombe cha chai kutwa mara tatu. Kanuni ya tatu: Chukua Bizrulqutni vijiko vitatu vikubwa uchemshe ndani ya maji lita moja na nusu. Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara mbili.


MARADHI YA MTU AU MTOTO KIKOJOZI: Kikojozi ni mtu ambae hukojoa kitandani usiku au mchana wakati anapokua amelala usingizi. Anaweza kuwa mtoto au mtu mzima SABABU: Sababu kubwa za mtu kuwa kikojozi ni pamoja na Kulegea kwa kibofu cha mkojo Kuota usingizini kuwa mtu anakojoa, na kuwa na usingizi mzito kuliko kiasi.

KULEGEA KIBOFU: Ikiwa kibofu cha mkojo kimelegea mkojo utakua hauna kizuizi cha kuzuia unapokua umeshakusanyika kwenye kibofu.

TIBA: Chukua asali nusu lita, unga wa kamun aswad vijiko sita vikubwa na unga wa habat soda vijiko vitatu vikubwa halafu ukoroge vyote pamoja. Chota vijiko viwili vikubwa vya mchanganyiko huu wa dawa ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili.

KUKOJOA KWA SABABU YA NDOTO: Sifa ya mtu anayekojoa kitandani akiwa usingizini anaweza akaota kuwa amekwenda chooni kukojoa lakini akiamka asubuhi anajikuta kuwa amekojoa kitandani, na anapokuwa anakojoa kitandani huwa anahisi raha wakati ule wa kukojoa.


SABABU: Hii huwa ni athari za ndoto za kishetani kwa sababu shetani humuotesha ndoto za kukojoa na akamkojoza kwa kihakika.
Hali hii pia huwatokea watu wazima bila kujali jinsia wala umri, wazima au wagonjwa

TIBA: FANYA HIVI Hakikisha umeshika udhu kabla ya kulala halafu usome kabla ya kulala Ayatul Qursii, Suratul-Ikhlas, Suratul Falaq na Suratul Nas mara tatu tatu kama inavyosema hadithi. Pia kabla ya kulala uombe dua ya kulala. Ukifanya hivyo shetani atakaa mbali nawe na ndoto hizi hazitatokea tena.

ANAEKOJOA KWA SABABU YA USINGIZI MZITO: Hali kama hii huwatokea watoto ambao hucheza sana mchana kisha wakachoka. Wanapoenda kulala huwa wamechoka sana na hata usiku wakati wamelala hawawezi kupata hisia ya kutaka kwenda kukojoa chooni kwa sababu wamezidiwa na usingizi.

TIBA: Tiba yake ni mtoto aweze kupunguza mchezo na aweze kulala kidogo mchana kama ilivyo katika mafundisho ya sunnah. Tiba ya pekee ni mtoto adhibitiwe na kupangiwa ratiba za kucheza, na kupangiwa muda wa kutosha kuweza kupumzika, ikiwezekana alale mchana kidogo.
mzizimkavu2009 is offline   Reply With Quote
Old 10-18-2011, 12:51 PM   #5
Salim
professional
 
Salim's Avatar
 
Join Date: Jan 2007
Location: Seeb, Oman
Posts: 295
Default

Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuhu

Asante sana ndugu Mzizimkavu kwa posts zako nzuri daima.

Shukran Wa baarakallahu fiik na salaam nyingi kutoka kwangu
Salim is offline   Reply With Quote
Reply

Thread Tools Search this Thread
Search this Thread:

Advanced Search
Display Modes

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off

Forum Jump

Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Nakuwa Na Hasira Sana Bila Ya Sababu, Nini Tiba Yake? Hilal Afya na tiba 2 03-12-2011 12:15 AM
Ewe Binaadamu Kwa Nini Unamuasi Mwenyezi Mungu Salim Ukumbi wa Dini 3 06-05-2010 12:17 AM
KILINGANISHWACHO NA BINAADAMU zanuba Ukumbi wa Dini 1 01-11-2010 10:09 PM
Wanawake Wananikimbia - Je, Jini Linaweza kumuoa Binaadamu? Mordiy Afya na tiba 0 11-26-2008 07:23 PM
50.HOJA ZINAZOWAFADHILISHA BINAADAMU WEMA KULIKO MALAIKA. rashid43 Ukumbi wa Dini 1 11-09-2008 12:51 AM


All times are GMT +4. The time now is 10:52 PM.

Powered by vBulletin® Version 3.8.3
Copyright ©2000 - 2016, Jelsoft Enterprises Ltd. Mahmoud Al-Asmi