Tuesday, 10 September 2019

Binadamu

MASIKINI MWANAADAMU,
KILA SIKU ANAPATWA NA MITIHANI MITATU!

Mtihani wa Kwanza;
Umri wake unapungua kila siku na wala hajali kwamba siku inapunguza umri wake.

Mali yake ikipungua anashughulishwa sana; ambapo mali inarudi; lakini umri haurudi.

Mtihani wa Pili.

Kila siku anakula riziki ya Allah Taala;
kama ni halali, ataulizwa kwa hayo; na kama ni haramu ataadhibiwa kwa hayo; na wala hajali matokeo ya hesabu.

Mtihani wa Tatu.

Kila siku anaikaribia Akhera kwa kiwango fulani; na anaiacha dunia kwa kiwango fulani; lakini pamoja na hayo; haipi umuhimu Akhera inayo mkaribia kama anavyoipa umuhimu dunia inayo maliza kwake;
Na wala hajui mwisho wake ni Pepo au Moto mkali.
Kutokana na kughafilika na Tamaa za kidunia na yaliyo kuwemo ...
Hali ya kuwa ni mapito mafupi tuu yasio kuwa na faida yoyote huko twendako zaidi ya Amali Njema...

Dini ni Nasaha ,,

Sunday, 8 September 2019

HII NAYO NI ADABU NJEMA


1. Usimpigie mtu simu kwa zaidi ya mara mbili mfululizo. Ukishaona simu yako haipokel'ewi basi elewa kuna sababu ya msingi acha subiri akupigie pindi atakapoona ulimtafuta.

2. Rejesha pesa ulizokopa bila kusubiri kukumbushwa na aliyekukopesha. Hiyo inaonesha uadilifu wako na tabia yako. Vivyo hivyo rejesha mwamvuri, peni, kitabu au chochote ulichoazima hata kama kidogo usisubiri kukumbushwa.

3. Usiagize chakula cha  gharama kubwa pale unapotolewa out na mtu. Ikiwezekana mwombe akuagizie mwenyewe au shauriana naye chakula gani unaweza kuagiza.

4. Usiulize maswali yenye ukakasi kama "Hee bado hujaolewa/hujaoa tu? Au " he! Hujapata mtoto tu?", "he! Hamjajenga tu? " Mwee bado tu hamjanunua gari?" Kwa kifupi ni kwamba hayakuhusu mhusika akipenda mjadili hilo ataanzisha mwenyewe.

5. Ikitokea unaingia mahali na kuna mtu anakuja nyuma yako ni vizuri ukamshikia mlango bila kujali umri au jinsia yake. Haikugharimu lolote kuonesha unajali.

6. Mkienda mahali na rafiki yako na akalipia usafiri au chakula basi jitahidi nawe kulipia zamu inayofuata usipende kupokea tu.

7. Kubaliana na mitazamo tofauti kumbuka 6 kwako inaweza kuwa 9 kwa aliyekaa upande mwingine. Mawazo ya ziada ni mbadala mzuri.

8. Usiwakatishe watu wanapokuwa kwenye mazungumzo yao mfano kwenye kundi kubwa la watu wao  wamejitenga pembeni wawili wanaongea jambo fulani wewe unajiingiza kwenye mazungumzo bila samahani na bila kukaribishwa.

9. Ukimtania mtu akaonesha kutofurahia acha mara moja na usirudie tena kumtania.

10.Sema Asante mtu anapokusaidia jambo lolote.

11.Msifie Mtu hadharani, mpinge faraghani.

12. Unapokutana na mtu huna sababu ya kukosoa uzito wake  "hee mbona umenenepa hivyo?" Au "Mbona umekonda sana?" Hayakuhusu akitaka kukueleza mwenyewe atakueleza wewe unatakiwa kusema tu  "Umependeza"

13. Mtu anapokuonesha picha kwenye simu yake usianze kwenda kushoto au kulia ili kutazama picha zingine ishia hiyohiyo anayokuonesha huwezi jua picha gani inafuata.

14. Mtu anapokuambia anakwenda hospitali usianze kumuuliza " una tatizo gani?" Haikuhusu akitaka atakuambia mwenyewe.

15. Mheshimu mfagizi kama unavyomheshimu boss maana heshima ni kitu cha bure.

16. Ongea na mtu huku unamtazama machoni sio kuwa bize na simu yako au kutazama pembeni.

17. Usitoe ushauri wowote kama hujaombwa kufanya hivyo.

18. Mkikutana na mtu usianze kumuuliza umri wake au kipato chake labda akuambie mwenyewe.

19.Vua mawani yako (kama ya urembo mf. ya jua) unapoongea na mtu.

20. Usiongelee mambo ya utajiri wako au mafanikio yako kwa watu wasio na uwezo wala mambo ya watoto wako kwa watu ambao hawajajaliwa watoto.
.
Mungu Akubariki wewe unaesoma ukiipenda share na wengine🙏🏼🙏🏼

Oman News

Middle East News

World News

Sports News

Business News

features