Tuesday, 30 January 2018

Wanaume na Wanawake wanaojihifadhi Tupu zao


DARSA YA KWANZA

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu): Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aina mbili za watu wa motoni siwaoni; Watu ambao wana fimbo (mijeledi) kama za mkia wa ng'ombe dume ambazo wanawapigia watu, na wanawake ambao wamevaa lakini wako uchi, wanawashawishi wanaume wawatongoze, na wanaelekea kwao (kwa kuwa warahisi). Vichwa vyao kama nundu za ngamia zinazoyumba. Hawataingia Peponi wala hawatasikia harufu yake ingawa harufu yake inaweza kunuswa kutoka masafa kadhaa na kadhaa)) [Muslim]  

Hadiyth hiyo ya Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inatudhihirikia uhakika wake kwani tunawaona dada zetu wengi wakidhani kuwa wamevaa mavazi ya hijaab na hali hawakutimiza hijab ya sheria inavyopasa. Utamuona mwanamke amejifunika kichwa tu lakini mwili wake wote haukusitirika kutokana na mavazi aliyovaa. Hivyo hudhani kuwa hijaab hasa ina maana ya kujifunika nywele pekee.

Basi hebu tutaje hapa hijaab ya Kiislamu inayotakikana kisheria:

1.  Nguo iwe ndefu ya kukufunika mwili mzima mpaka miguu, na kama ni fupi kidogo basi uvae soksi. Ukivaa nguo ambayo itaonyesha sehemu yoyote ya mwili isipokuwa uso na viganja, basi utakuwa hukuvaa hijaab sawa sawa

2.    Nguo hiyo iwe pana na sio yenye kuonyesha umbo lako, yaani isiwe yenye kukubana popote mwilini khaswa kuanzia kifuani hadi magotini.

3.    Nguo iwe nzito na si nyepesi yenye kuonyesha mwili wako, yaani kitambaa cha nguo kisiwe chepesi.

4.    Kutokuvaa nguo zinazofanana na nguo za kiume.

5.    Kutokuvaa nguo zenye urembo sana za kuvutia  

6.    Kutotia manukato.

Dada zetu wa Kiislamu watakapotimiza haya watakuwa wamekamilisha hijaab zao na watakuwa katika stara pamoja na kusitiri jamii na ndipo watakapokuwa wamejitahidi kujihifadhi waweze kuingia katika sifa hiyo ya kuhifadhi tupu zao Insha Allah.```

Itaendelea In shaaa ALLAH

*☎+97433799776*

NDOA KATIKA UISLAM
📗〽〽〽〽〽〽〽〽〽📗

VIAPO NA  AHKAAM ZAKE

🔵🔴🔵🔴🔵🔴🔵🔴🔵

Amesema Allah subhaanahu wata'alaa, ktk surati Almaaida aya (89)

لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أيْمَانِكُمْ وَلَٰكِنْ يُؤَاخِذُكُمْ بِمَا عَقَّدْتُمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِمَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُون 89

📓 MAANA  YAKE 📓

((_Mwenyezi Mungu hatakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni kwa mnavyo apa kweli kweli kwa makusudio. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacho walisha ahali zenu, au kuwavisha, au kumkomboa mtumwa. Asiye pata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapo apa. Na hifadhini yamini zenu. Namna hivyo Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake ili mpate kushukuru_))

📓 MAFUNZO  YAKE📓:-

✍  Bila shaka aya inatupa wazi hukmu ya kiapo cha mtu kukusudia na nini hukmu yake au kafara yake

kwa ufupi:!
☝Kiapo
maana yake kilungha
ni "mkono wa kulia ,kwani inasemekana kuwa walikuwa warab wanapoapa basi kila mmoja huukamata mkono wake wa kulia ,na wako waliosema kuwa mkono wa kulia kawaida ni mkono wenye kuhifadhi na kulinda kila kitu.

Amma kisheria kiapo maana yake ni "

تَوكيدُ القولِ بِذكر إسم مِنْ أسماء الله أو صفة من صفاته
_Kuitia mkazo qauli yako kwa kutaja jina miongon mwa majina ya Allah au sifa zake_

📝 AINA ZA VIAPO📝

➡:-Na viapo anavoapa binadamu viko aina mbili kuu

1⃣)- Kiapo cha upuuzi
2⃣)- Kiapo cha kukusudia

1⃣ KIAPO CHA UPUUZI

  kiapo cha upuuzi bila wewe kukusudia ndani ya moyo wako ...
wako baadh ya maulama waliosema nikiapo cha kuhalalisha kile alichoharamisha Allah

ndio walipotaka kujua hukmu yake nini wafanye wakenda kwa mtume s.w.a wakasema

يا رسول الله كَيفَ نَصْنعُ بأيماننا التي حَلَفنا عليها
"Ewe mjumbe wa Allah nin tufanye sasa juu ya viapo vyetu?""

hapo ndio Allah akateremsha aya hii

لا يُواخِذكمُ اللهُ باللغو في أيمانكم
"
Allah hatakushikeni ktk viapo vyenu vya upuuzi"

na wako waliosema kuwa viapo vya kipuuzi ni kusema

لا والله ، بلى واللهِ ، واللهِ ، وكلا ، والله
"sivo nakuapia" "kwanini isiwe hivo naapa kwa mungu" sio hivo voo naapa kwa mungu"

☝na wako walisema inakuwa  kwa mfano kusema hali umekasirika na ghafla tu bila wewe kujitambua

📝 HUKMU YA KIAPO
   *CHA UPUUZI* 📝

✍viapo kama hiv ni : kuwa huna kosa wala hutoi kafara .kwa vile hujavikusudia ndani ya moyo wako ...

  2⃣:- KIAPO CHA    KUKUSUDIA

viapo vya kukusudia hassa ndani ya moyo wako
kwa mfano :-

naapa kwa jina la Allah sitofanya tena jambo hili , kisha ukafanya,
au ukasema " naapa nitafanya kitu flani , kisha baadae asifanye....

📝 HUKMU YA KIAPO
   CHA KUKUSUDIA📝

hii☝� hukumu yake kama hujavitekeleza jinsi ulivoapa na muda uliouanisha basi utapaswa kutoa
        👇👇👇👇👇
((kafara mursala ))

  ▶ Jinsi ya utekelezaji wa kafara hii :-

1)-إطْعامُ عشَرَةِ مساٍكيْنَ مِنْ أوسط ما تُطْعِمُونٍ أهليكم أوْ كِسْوَتُهم"

"Kuwalisha maskini kumi ,kwa chakula cha wastani munachowalisha watu wenu au kuwavisha "".

na kama hakuweza basi atafanya jambo hili 👇

2)- أوْ تَحْريرُ رَقَبَة

"au kumkomboa mtumwa"

na kama hakuweza kufanya mambo yoote mawili basi atafanya jambo hili la mwisho 👇

3)- فَصِيامُ ثَلاثَةِ أياّمِ،

"atafunga siku tatu kwa mfulilizo""

▶ Ndung zangu tuzilinde na kuzihifadhi viapo vyetu kwa utaratibu uliowekwa pindi tunapomuapia Allah na kumpa ahadi ya kiapo,
na tujiepushe na viapo vya upuuzi ili tufanikiwe dunian na akhera.
 
والله أعلم
By:-

✍Humoud Alrawaahiy
+96894646722/Oman

📲Facebook~
Sheikh Humoud Alrawaahiy
_________________________

يَوْمُ الأربعاَء: ١٣/ جُمَادى الأُولى/١٤٣٩
Jumatano :-31/01/2018

Oman News

Middle East News

World News

Sports News

Business News

features