Monday, 3 October 2016

Umoja ni nguvu

NITAPIGANIA UMOJA WETU MPAKA PUMZI YA MWISHO


tuone yanayotukusanya

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنْتُمْ مُسْلِمُون

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife ila nanyi ni Waislamu.

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنْتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنْتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِ فَأَنْقَذَكُمْ مِنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ

Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

*Wala msiwe kama wale walio farikiana na kukhitalifiana baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa*.

OMBI LA WAISLAMU
WOTE ULIMWENGUNI

HAKUNA KAZI MUHIMU TUNAYO WAOMBA MASHEKHE NA MUFTI WA DUNIA NZIMA KULIKO KUTULETEA UMOJA WETU ULIOPOTEA.

Tunakuombeni :

1. WEKENI MADHEHEBU ZENU KANDO (sababu ya kukusanya )

(Tunapoutafuta umoja)

2. KUWENI WAISLAMU TU

3. TANGULIZENI SABABU ZA KUTUKUSANYA.(zipo nyingi):

a] nguzo za uislamu
b] nguzo za imani
c] kibla yetu ni moja
d] Qurani ni moja
e] mtume WETU ni mmoja
f] Dini ni moja
g] Sala 5
h] ramadhani na idi zetu

(kama mtashindwa)

4. ACHENI SABABU ZA KUTUFARIKISHA. (Nazo ni chache)

5. FANYIANENI DHANA NJEMA NYINYI KWA NYINYI.

6. LENGO LENU LIWE NI MOJA TU (UMOJA WETU)

TUMECHOKA MFARAKANO TUITIKIENI NA SISI

Waislamu je mnaniunga mkono?

كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَهُمْ ۚ مِنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.

ADUI HAJALI MADHEHEBU YEYE ANAPIGA VITA WAISLAMU TU!

Imeandikwa na mpenda umoja wa umma:

Rashid shukery

Mkono kwa mkono hadi tufikie umoja wetu


Sunday, 2 October 2016

Mwaka mpya, nguvu mpya


Mambo ambayo Tunatakiwa Kujiepusha Nayo katika maisha yaliyobakia;
1-Kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama kufanya uchawi, kuwaendea waganga, watabiri, kutufu makaburini, na mengineyo ya shirki
2-Kuzini
3-Kulewa
4-Kuiba na kumdhulumu mtu haki yake
5-Kugombana, kutukanana, kuvunjiana heshima, kudharauliana n.k.
Kusengenya (Ghiybah).
Tv-Kusema uongo, na kila aina ya uovu mwengine.
Mambo ambayo Tunatakiwa Kuzidisha Kutenda;
1- Swalaah na Swalaah za Sunna.
2-Kufunga Swawm Jumatatu na Alkhamiys, Masiku meupe (Ayyaamul-biydhw) (tarehe 13, 14 na 15) na Swawm ya Nabiy   Daawuwd (kufunga kila baada ya siku moja).
3-Kutafuta ‘ilmu ya Dini kwa kusoma na kusikiliza mawaidha.
4-Kuomba maghfirah na kutubia (tawbah).
5-Kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa wingi kwa tasbiyh (Subhaana Allaah), tahmiyd (AlhamduliLLaah) tahliyl (laa ilaaha illa Allaah takbiyr (Allaahu Akbar).
6-kusoma Qur-aan, kumshukuru na kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
7-Kuunga undugu, kwa kuwasiliana na ndugu, jamaa na kila anayemuhusu mtu kwa damu.
8'Kuwafanyia ihsaan wazazi wawili.
9-Kuwafanyia ihsaan majirani, marafiki na Waislamu kwa ujumla.
10-Kutoa Swadaqah.
11-Kulisha maskini.
12-Kusuluhisha waliokhasimikiana.
13-Kuamrishana mema na kukatazana maovu.
Amali njema yoyote ile usiache kuitekeleza ee ndugu Muislamu hata   iwe   ndogo vipi kwa sababu hujui* *‘amali ipi itakayokupatia radhi za Allaah (‘Azza wa Jalla)ikawa sababu ya kuingia kwako Jannah. Kumbuka Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Imepokelewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Usidharau kufanya jambo jema lolote lile hata ikiwa kukutana na nduguyo kwa uso wa bashasha))
[Muslim]
(Mwaka mpya nguvu mpya).
Imani haizeeki.
fikishwa yaliyofikishwa.
Mkono kwa Mkono Hadi Peponi.
Sheikh Rashid Anaomba tubadilike.

Oman News

Middle East News

World News

Sports News

Business News

features